BiasharaMilele FmSwahili

Wateja wa Mpesa kuanza kutumia PayPal

Paypal na Safaricom zimeafikia makubaliano ya kuwawezesha wateja wake kuhamisha pesa kati ya huduma yake ya mpesa na PayPal. Makabaliano hayo yanasaidia kuondoa vikwazo vilivyokuwepo kwa wateja wa mpesa kutumia fursa hiyo ya kutuma na kupokea fedha katika ya mataifa tofauti ya PayPal. Efi Dahan meneja mkuu wa PayPal barani Afrika na Urusi anasema wateja sasa wataweza kuondoa na kuweka fedha kwenye mfumo huo wa kutumia na kupokea pesa kwa njia ya dijitali.

Show More

Related Articles