HabariPilipili FmPilipili FM News

MwanaFunzi Wa Darasa La Saba Apatikana Na Bastola.

Maafisa wa polisi kaunti ya Kilifi wamefanikiwa kupata bastola mbili na risasi kumi na moja zilizokuwa zinamilikiwa na wananchi kwa lengo la kutekeleza uhalifu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Akidhibitisha hilo kamanda wa polisi eneo hilo Fredrick Ochieng amesema moja kati ya bastola hizo ilipatikana mikononi mwa mwanafunzi wa darasa la saba anaesoma katika shule ya msingi ys Mikanjuni eneo la Takaungu ndani ya kaunti hiyo.

Ochieng ameendelea kuelezea kuwa bastola ya pili imepatikana kutoka mikononi mwa wahalifu waliojaribu kumuibia mfanyibiashara mmoja kabla ys mmoja wao kuchomwa na wananchi waliojawa ghadhabu huku mwengine akifanikiwa kutoroka.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Show More

Related Articles