HabariMilele FmSwahili

Spika wa Seneti ajitenga na madai kuwa alichochea kutimuliwa kwa Wetangula kama kiongozi wa wachache

Spika wa seneti Ken Lusaka amejitenga na madai alichochea kutimuliwa seneta wa Bungoma Moses Wetangula kama kiongozi wa wachache. Akiongea baada ya kufunga kongamano la viongozi wa bunge la seneti huko Naivasha, Lusaka anasema ni maseneta wa ODM waliidhinisha kubanduliwa kwa Wetangula na yeye aliridhia uamuzi wao wa kumchagua seneta wa Siaya James Orengo kujaza wadhfa huo. Amesema jukumu lake ni kutoa uongozi usio wa mapendeleo kuhakikisha maseneta wanafanikisha majukumu yao.

Aidha, Lusaka amedhibitisha maseneta wote wameagizwa kuhudhuria kongamano la magavana litakalofanyika mjini Kakamega baadaye mwezi huu ili kujadiliana jinsi watashirikiana kufanikisha ugatuzi.

Show More

Related Articles