HabariMilele FmSwahili

“Kati ya wakenya 5 nchini, 4 hawana bima ya afya”

Kati ya wakenya 5 nchini 4 hawana bima ya afya. Takwimu za wizara ya afya zinaashiria kila mwaka zaidi ya wakenya milioni 1 hufilisika kutokana na gharama ya juu ya tiba. Waziri Sicily Kariuki anasema serikali inajitahidi kuhakikisha takwimu hizi zinabadilika kutokana na mipangilio inayowekwa na rais Uhuru Kenyatta. Takwimu hizi zinawadia huku ulimwengu kesho ukiadhimisha siku ya afya ulimwenguni kauli mbiu ikiwa afya bora kwa gharama nafuu

Show More

Related Articles