HabariMilele FmSwahili

Mwanamume wa miaka 30 alazwa hospitalini baaba ya kumeza mswaki Mombasa

Mwanamume wa miaka 30 amelazwa hospitali Mombasa baada ya kumeza mswaki. David Charo anadai mswaki huo ulimteleza na kuumeza. aidha kulingana na binamuye , James Katana, kwa siku tano wamesalia hospitalini humo na mgonjwa huyo hajapokea matibabu licha ya uchunguzi wa madakatari kuonyesha mswaki huo uko tumboni. Wanataka upasuaji wa haraka kufayiwa jamaa wao ili kuuondoa mswaki huo.

Show More

Related Articles