HabariMilele FmSwahili

Eneo maalum kutengewa magari ya uchukuzi wa umma katika barabara kuu ya Thika

Barabara kuu ya Thika itakuwa na eneo maalum litakalotengewa magari ya uchukuzi wa umma. Waziri wa uchukuzi James Macharia ameielezea kamati ya seneti ya uchukuzi kuwa hatua hii inatarajiwa kupunguza msongamano wa magari jijini. Aidha amesema mpango huo umeanza kutekelezwa mara moja.

Macharia pia amewataka wadau katika sekta ya uchukuzi kukumbatia matumizi ya mabasi ya NYS kusafirisha umma.

Aidha amedokeza mamlaka ya bara bara kuu KENHA huenda ikajenga bara bara mpya ya Mai Mahiu Narok kutokana na bara bara hiyo kuwa na mtaro.

Show More

Related Articles