HabariMilele FmSwahili

Polisi muuaji almaarufu Katitu ahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani

Titus Musila almaarufu Katitu ambaye ni afisa wa polisi aliyetuhumiwa kwa kumuua jamaa wa miaka 27 amehukimiwa kifungo cha miaka 15 gerezani. Jaji James Wakiaga amemhukumu Musila kuhudumia kifungo cha miaka 12 gerezani na miaka 3 kifungo cha nje na huduma kwa jamii. Hata hivyo amempa ruhusa musila kukata rufaa iwapo anahisi kutoridhishwa na hukumu hiyo.

Musila amekua rumande tangu mwaka 2014 alipokamatwa kwa kosa la kumuua jamaa huyo aliyeripotiwa kuwa mwizi. Kukamatwa kwake kulisababisha maandamano makubwa eneo la Githurai hapa Nairobi ambapo alikua akihudumu,wenyeji wakitaka aachiliwe huru kwa madai alisaidia kuwaangamiza majambazi eneo hilo.

Show More

Related Articles