HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mahame ya Mlima Elgon: Wakazi wametorokea maeneo salama kwa kuhofia usalama wao

Wakaazi wa Mlima Elgon aidha waliukaribisha mwaka mpya kwa maafa huku watu 37 wakiuwawa katika kile kinachoaminika kuwa mzozo wa ardhi.

Mauaji hayo sasa yakipelekea serikali kuweka marufuku ya kutotoka nje kwa siku 90 huku serikali ikisaka mshukiwa wa kundi haramu la g-5 Timothy Kiptanui kitai, al maarufu Cheparkach ambaye amehangaisha maisha ya maelfu ya wakaazi wa Mlima Elgon.

Mwanahabari wetu Shukri Wachu alizama eneo hilo na sasa ameibuka na taarifa kuhusu eneo ambalo sasa limesalia mahame.

Show More

Related Articles