HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mifugo walioibwa wachinjwa na kuuzwa Kamulu-Machakos

Wenyeji wa kijiji cha Kantafu eneo la Kamulu kaunti ya Machakos wanaishi kwa hofu kufuatia msururu wa visa vya wizi wa ng’ombe eneo hilo ambao hatimaye huchinjwa na mizoga yake kutupwa kiholela.

Juma lililopita ng’ombe wanne walipotea pamoja na punda mmoja na mizoga kupatikana baadaye.
Haya yanajiri huku boma kadhaa zikisalia na zizi lisilokuwa na ng’ombe kufuatia wizi huo.

OCPD wa Matungulu Samuel Mukuusi amesisitiza kuwa maafisa wa polisi wanaendelea na msako na kwa sasa mshukia mmoja amekamatwa.

Show More

Related Articles