HabariMilele FmSwahili

Boinet aitetea idara ya polisi dhidi ya tuhuma za kuwa fisadi zaidi nchini

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet ameitetea idara yake dhidi ya tuhuma za kuwa fisadi zaidi nchini. Boinnet aliyefika mbele ya kamati ya seneti kuhusu uchukuzi amesema maafisa wote waliohusishwa na kashfa za ufisadi wamekabiliwa kwa mujibu wa sheria. Boinnet anasema kufikia sasa afisi yake kwa ushirikiano na tume ya huduma kwa polisi imewafuta kazi zaidi ya maafisa 300 wafisadi. Aidha amewaraia wakenya kukoma kutoa hongo ili kupokea huduma muhimu kutoka kwa maafisa wa polisi

Show More

Related Articles