HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta awaonya maafisa wa serikali wanaojihusisha na ufisadi

Kwa mara nyingine tena rais Uhuru Kenyatta amewaonya maafisa wa serikali wanaojihusisha na ufisadi kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria. Akizungumza baada ya kuongoza ufunguzi wa kliniki ya macho na meno katika hospitali ya Tenwek kaunti ya Bomet rais Kenyatta amesema hatawavumilia watu fisadi wanaohujumu juhudi za serikali kufanikisha maendeleo.
Rais Kenyatta pia amesema serikali itafungua kliniki sawia kaunti za Mombasa na Uasingishu baadaye mwaka ujao ili kuboresha huduma kwa wagonjwa.
Naye naibu rais William Ruto amesema vituo vya afya vya umma na kibinafsi vitashirikiana katika kutoa huduma ya afya kwa wote.

Show More

Related Articles