HabariPilipili FmPilipili FM News

Waziri Wamalwa Akutana Na Raila.

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa leo anakutana na kiongozi wa NASA Raila Odinga kujadili maswala ya ugatuzi.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na naibu mwenyekiti wa baraza la magavana nchini  Anne Waiguru, na naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ugatuzi seneta Irungu Kangata.

Viongozi hao wanatarajiwa kumjuza Raila kuhusiana na maandalizi ya kongamano la kitaifa la ugatuzi, litakaloandaliwa kaunti ya kakamega tarehe 23 hadi 27 mwezi huu.

Show More

Related Articles