MichezoMilele FmSwahili

Starlets kuchuana na Uganda kwenye mechi ya kufuzu AWCON

Vipusa wa Harambee Starlets hii leo wanakutana na warembo wa Uganda kwenye mgaragazo wa raundi ya kwanza wa kutafuta nafasi kufuzu kushiriki mechi za kuwania timu bingwa barani Afrika .

Nahodha wa vipusa Wendy Achieng’  ana imani kwamba watafanya vyema kwenye mechi hiyo .

Iwapo Starlets watashinda watakutana na Equatorial Guinea kwenye raundi ya pili , raundi itakayowapa tiketi ya kufuzu iwapo watashinda . Mechi hiyo inang’oa nanga saa tisa kamili ugani Machakos .

Show More

Related Articles