MichezoMilele FmSwahili

Mathare United kuchuana na Nakumatt FC ugani Ruaraka leo

Vijana wa mtaa Mathare United hii leo wana fursa ya kuwabandua viongozi wa jedwali la ligi kuu KPL Gor Mahia kidedeani mwa jedwali wanapokutana na Nakumatt FC ugani Ruaraka .

Mathare ni nambari mbili kwenye jedwali na pointi 17 mbili nyuma ya Kogalo ambao hawana mechi wiki hii kwani wanajitayarisha kuchuana na Supersport United ya Afrika kusini siku ya Jumamosi kwenye mgaragazo wa mashirikisho barani Afrika .

Mechi hiyo itang’oa nanga mida ya saa nane kamili ugani Ruaraka kisha saa kumi dakika 15 Batoto ba Mungu Sofapaka wasakate dhidi ya Nzoia Sugar .

Kwenye mitanange mingine hii leo

Chemelil Sugar FC vs Thika United – Chemelil Complex – 1PM

Posta Rangers vs Kakamega Homeboyz – Camp Toyoyo – 3PM

Ulinzi Stars vs Vihiga United – Afraha Stadium – 3PM

Show More

Related Articles