HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Makataa yaondolewa kwa usajili wa wanafunzi kwa mfumo wa NEMIS

Ni afueni kwa walimu na wazazi baada ya wizara ya elimu hii leo kutangaza kwamba wanafunzi ambao hawajajisajili kwenye mfumo wa kidijitali wa kuwatambua wanafunzi- NEMIS, wanaweza kufanya hivyo bila wasiwasi wowote.
Waziri wa Elimu Amina Mohammed ameyasema haya baada ya kupokea malalamishi kwamba wanafuzi wengi hawakuweza kujisajili kutokana na ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa miongoni mwa changamoto nyingine.
Hadi sasa wanafunzi milioni 6.3 wamesajiliwa katika shule za msingi na wanafunzi milioni 3 kusajiliwa kwenye mfumo huo wa NEMIS kwa shule za upili.

Show More

Related Articles