HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Matiang’i ajiondolea lawama kuhusiana na masaibu ya Miguna JKIA

Waziri wa usalama Dkt Fred Matiangi sasa anailaumu idara ya mahakama kwa madai ya kushirikiana na mashirika ya kijamii kudhalilisha maafisa wa serikali.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, Matiang’i amesema imekuwa vigumu kutekeleza majukumu serikalini kutokana na amri zinazotolewa na mahakama huku na kule ya hivi punde ikiwa ni amri iliyotolewa ya kuachiliwa kwa wakili Miguna Miguna.

Matiang’i ameyasema haya siku chache tu baada ya kudinda kufika mahakamani kama alivyotakiwa kueleza ni kwa nini wakili Miguna Miguna hakukubaliwa kuingia nchini.

Show More

Related Articles