HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta arejea nchini baada ya kukamilisha ziara nchini Msumbiji

Rais Uhuru Kenyatta amerejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya siku nne nchini Msumbiji. Ziara iliyotumika kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya Kenya na Msumbuji. Rais Kenyatta na mwenyeji wake Filipe Nyusi walishuhudia utiaji saini makubaliano kuhusu ushirikiano katika maswala ya kibiashara uchimbaji madini utalii na kilimo biashara. Ni katika maafikiano hayo ambapo Kenya itafungua ubalozi wake msumbiji hivi punde pamoja na kuwaruhusu raia wa mataifa haya kuzuru Kenya na msumbiji bila kuhitaji visa.

Show More

Related Articles