HabariMilele FmSwahili

Mshukiwa anayedaiwa kuwatapeli wabunge Wazir Masubo kusalia rumande kwa siku nne

Mshukiwa anayedaiwa kuwatapeli wabunge Benson Wazir Masubo atazuiliwa rumande kwa siku nne. Hii ni kufuatia agizo lililotolewa na hakimu mkaazi wa mahakama ya Milimani Christine Njagi. Hakimu Njagi ameagiza mshukiwa huyo aliyefikishwa mahakakani leo kufanyiwa uchunguzi wa akili katika hospitali ya Mathare. Alikamatwa wikendi iliopita huko Tarime nchini Tanzania akidaiwa kuwa safarini kuelekea nchini Congo.

Show More

Related Articles