HabariPilipili FmPilipili FM News

Wagonjwa Wa Kifua Kikuu Hawafuatilizi Matibabu Yao Vipasavyo Kwale

 

Asilimia 15  ya wagonjwa wa kifua kikuu kaunti ya Kilifi hawafuatilizi matibabu ipasavyo.

Haya yamebainishwa na waziri wa afya katika kaunti hiyo Dakitari Anisa Omar.

Anisa anasema wagonjwa hao hushindwa kumalizia matibabu baada ya kupata afueni kidogo jambo ambalo anasema ni hatari kwa afya yao.

Amewataka wananchi wenye dalili za kifua kikuu kutembelea hospitali katika kaunti hiyo ili waweze kuchunguzwa endapo wanaugua ugonjwa huo au la.

Wizara hiyo pia imeanzisha mpango maalumu ambao unalenga kuimarisha huduma za afya mashinani katika kaunti hiyo.

Show More

Related Articles