HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wiper kujibadili na kuwa vuguvugu la ‘One Kenya Movement’ OKM

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ametangaza kwamba atabadili chama hicho na kuwa vugu vugu kwa jina One Kenya Movement, OKM.

Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa jamii ya wakamba eneo la Matungulu kaunti ya Machakos, Kalonzo pia amesema anaamini atakuwa rais wa tano wa Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2022.

Akizungumza katika hafla hiyo, aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama ameitaka jamii ya wakamba kumuunga mkono Kalonzo katika kampeni yake ya urais mwaka wa 2022.

Show More

Related Articles