HabariMilele FmSwahili

Makataa ya basi za shule kupaka rangi ya manjano yakamilika rasmi

Makataa iliotolewa kwa shule zote kupaka mabasi ya shule rangi ya manjano imekamilika rasmi. Wizara ya elimu inatarajiwa kuanzisha msako mkali kwa shule ambazo zimepuuza makataa hiyo. Mwaka jana, aliyekua waziri wa elimu dr.Fred Matiang’ aliagiza mabasi yote ya shule kupakwa rangi ya manjano ili kurahisisha kutambuliwa kwa mabasi hayo ambayo yalikua yanatumiwa kwa shuguli zisizostahili. Agizo hilo lilifuatia sheria iliopasishwa na bunge kutaka mabasi ya shule kuwa na rangi maalum kama mataifa mengine. Hata hivyo tayari baadhi ya wadau katika sekta ya elimu wametaka makataa hiyo kuongezwa wakidai kutokua na fedha za kutekeleza agizo hilo.

Show More

Related Articles