HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta atuma ujumba wa heri njema kwa rais mpya wa Botswana Mokgweetsi Masisi

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa heri njema kwa rais mpya wa Botswana Mokgweetsi Masisi anapoanza utawala wake. Katika ujumbe wake rais Uhuru anasema kuchaguliwa kwake kumedhihirisha imani walio nao raia wa Botswana katika uongozi wake. Rais ambaye alizuru Botswana mwaka wa 2016 anasema mataifa haya mawili yamekuwa na uhusiano bora kwa muda huku akitoa mwaliko kwa rais Masisi kuzuru Kenya. Amempongeza pia rais anayeondoka Seretse Khama Ian Khama kwa kukubali kumkabidhi Masisi mamlaka.

Show More

Related Articles