HabariMilele FmSwahili

Viongozi wa Ukambani wakutana kutia saini mkataba utakaotoa mwelekea wa kisiasa wa jamii ya Wakamba

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka Charity Ngilu wa Narc Kivutha Kibwana na Johnstone Muthama wanaongoza viongozi kutoka jamii ya akamba kutia saini kwenye mkataba utakaotoa mwelekeo wa kisiasa kwa jamii hiyo. Mkao huo unaoandaliwa katika shule ya msingi ya kiamba Komarok kaunti ya Machakos unahudhuriwa pia na viongozi wa kidini wasomi wataalam na wanasiasa. Wanachama wa chama cha Wiper NARC muungano wanahudhuria mkao huo. Hata hivyo chama cha Maendeleo Chap Chap kimejitenga na mkutano huo kwa madai kuwa hawakuhusishwa. Mkutano huo utatumika kumpa mwelekeo wa kisiasa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Show More

Related Articles