HabariMilele FmSwahili

Mwanamme anayetuhumiwa kuwalaghai wabunge anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga

Mwanamme ambaye anatuhumiwa kuwalaghai wabunge anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga. Hii ni baada yake kuhojiwa katika makao makuu ya CID. Wazir Masubo Chacha alikamatwa huko Tarime Tanzania kufuatia oparesheni iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya maafisa wa Kenya na Tanzania. Chacha anadaiwa kutumia jina la mwakilishi kina mama huko Muranga Sabina Chege kuwalaghai wabunge.

Show More

Related Articles