HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Tobiko ahojiwa kwa kuwafuta maafisa wa KFS

Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko hii leo amefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu mazingira inayoongozwa na Mbunge wa Maara Kareke Mbiuki, alikotakiwa kuelezea ni kwa nini aliwasimamisha kazi baadhi ya maafisa wa shirika la kulinda misitu KFS.

Tobiko aliiambia kamati hiyo kuwa majina ya maafisa hao wa KFS waliosimamishwa kazi yalitolewa na mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo.

Wakati huo huo Tobiko aliongeza kuwa wanajeshi wa humu nchini wamejitolea kwa shughuli ya upanzi wa miti katika misitu iliyoharibiwa pakubwa.

Show More

Related Articles