HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika: Ukakamavu wa Mwalimu Mkuu anayepiga vita ndoa za mapema, Baringo

Kwenye makala ya wasiotambulika hii leo tunafululiza hadi Chemolingot eneo bunge la Tiaty, kaunti ya Baringo.

Hapa kuna mwalimu mkuu kwa jina Florence Lomariwa, mwalimu huyu anaongoza shule mbili kwa mpigo shule ya msingi ya Chemolingot, na shule ya upili ya Chemolingot lakini si hayo tu, mwalimu huyu ametenga darasa moja na kulifanya makao ya wasichana wanaotoroka tohara na ndoa za mapema vijijini.

Anawafunza yeye, kuwalisha na kuwalinda dhidi ya tamaa ya wazee wa eneo hilo wanaowamezea mate wakitaka kuwaoa kwa lazima.

Huyu hapa Dennis Matara na makala ya Wasiotambulika.

Show More

Related Articles