HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Shule zasalia na siku 2 kupaka mabasi rangi ya manjano

Huku ikisalia siku mbili shule kutii makataa ya wizara ya elimu kupaka mabasi ya  wanafunzi rangi ya manjano kote nchini  walimu wakuu wanajizatiti kuhakikisha kwamba wameafikia mapendekezo ya wizara.

Wizara hiyo mapema mwaka huu iliagiza kwamba rangi itakayotumika italazimika kutokuwa na chembe chembe za madini ya risasi au “lead” kwa kimombo na pia jina la shule kuandikwa kwa herufi kubwa za rangi nyeusi pembeni mwa basi.
Na huku muhula wa kwanza ukitarajiwa kukamilika idadi kubwa ya shule zimeafikia mapendekezo hayo ingawaje zipo baadhi ya shule ambazo hazijatii amri hiyo.

Show More

Related Articles