HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mahakama Kuu yawapiga faini Matiang’i,Boinnet na Kihalang’wa ya Ksh 200,000  

 

Mahakama kuu sasa imewapiga faini ya shilingi elfu mia mbili waziri wa usalama Fred Matiangi, inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugenzi wa uhamiaji Gordon Kihalang’wa kwa kukiuka maagizo ya mahakama.

Jaji George Odunga aliyetoa uamuzi huo, amesema faini hiyo itakatwa kutoka kwa mshahara wa mwezi ujao kwa kila mmoja wa watatu hawa.

Jaji Odunga hakueleza kuhusu hatima ya kesi ya kuzuiliwa kwa Miguna Miguna akihofia kutoa ilani itakayokiukwa.

Show More

Related Articles