HabariMilele FmSwahili

Mahakama yawatoza faini ya shilingi eflu 200 Matiangi, Boinnet na Kihalangwa

Mahakama imewatoza faini ya shilingi elfu  200 kila mmoja waziri wa usalama dr Fred Matiangi,inspecta generali wa polisi Joseph Boinett na katibu wa uhamiaji major mstaafu Kihalangwa. Jaji George Odunga anasema fedha hizo zinafaa kukatwa kwenye mishahara yao ya mwezi huu kwa kuikuka maagizo ya kufika mbele yake kujibu mashtaka ya kumzuilia kinyume na sheria Miguna Miguna
Odunga anasema haitokuwa vyema kwake kukubali wito wa mawakili wa Miguna kwamba wananchi wanafaa kuwakamata maafisa hao kwani wanaofaa kuhakikisha wanatiwa mbaroni ni maafisa wa ngazi ya chini
Kadhalika jaji Odunga aliyeelezea kukerwa na maafisa hao wakuu wa serikali hata hivyo amektaa kutoa agizo la kuwataja kama wasiofaa kushikilia nafasi za uongozi

Show More

Related Articles