HabariPilipili FmPilipili FM News

Waziri Fred Matiang’i Atandikwa Faini Na Mahakama.

Mahakama kuu imewaamuru waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi, ,inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkuu wa uhamiaji Gordon Kihalangwa kulipa faini ya shilingi elfu 200 kila mmoja kwa kukiuka agizo la mahakama.

Akisoma uamuzi huo, jaji George Odunga anasema watatu hao wanafaa kuwasilisha faini hiyo la sivyo itakatwa moja kwa moja kutoka kwa mishahara yao ya mwezi ujao baada ya kupatikana na hatia ya kukaidi agizo la kufika mbele ya mahakama.

Amesema hakuweza kutoa amri ambayo haiwezi kutekelezwa ndipo akaamua kuto agizo la kulipwa faini.

Hii ni baada ya watatu hao kukosa kumuwasilisha Miguna Miguna mahakamani humo na hata wao kukosa kufika kama walivyoagizwa.

Kwa sasa Miguna Miguna anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja Dubai baada ya kudaiwa kuleweshwa kabla ya kusafirishwa nchini humo jana usiku.

Show More

Related Articles