HabariMilele FmSwahili

ODM yatishia kuongoza umma kuwakamata na kuwawasilisha Matiangi, Kinoti, Boinnet na Kihalangwa wiki ijayo

Chama cha ODM sasa kinatishia kuongoza umma juma kesho kuwakamata na kuwawasilisha mahakamani dr Fred Matiangi, mkuu wa mkuu wa idara ya jinai George Kinoti,inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na katibu wa uhamiaji Gordon Kihalangwa wanaokabiliwa na kesi ya kukaidi maagizo ya mahakama. Katika taarifa ODM imewasuta 4 hao kwa kutumia mmalaka zao vibaya. Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na katibu wa ODM Edwin Sifuna, ODM inataka jaji mkuu Davaid Maraga kuwazuia 4 hao dhidi ya kusaka haki katika mahakama zozote nchini hadi pale watakaporidhia maagizo ya mahakama kwa kumrejesha nchini Miguna Miguna. Aametaka katiba kufuatwa kwa kuhakikisha wanne hao wanaondolewa afisini.

Show More

Related Articles