HabariMilele FmSwahili

Seneta McCarter anatarajiwa kumridhi Godec kama balozi wa Marekani nchini

Senata Kyle McCarter antarajiwa kuchukuwa rasmi mamlaka kama balozi mpya wa Marekani nchini. Ni kufuatia tangazo la rais Donald Trump kuwa amemteua McCater kuchukuwa mahala pa Robert Godec. McCater ni seneta wa jimbo la Illinois tokea mwaka wa 2009. Kati ya mwaka 1984-1989, alihudumu kama mkurugenzi wa shirika moja la kimisaada katika eneo la Mukithoma kaunti ya Tharaka Nithi. Balozi anayeodoka Godec aidha amesifia juhudi zake katika kuimarisha uhusiano wa Kenya na Marekani. Kwenye taarifa Godec ametaja kunawiri kwa sekta za afya elimu kilimo uwekezaji na usalama kama baadhi ya mafanikio ya uongozi wake nchini.

Show More

Related Articles