MichezoPilipili FmPilipili FM News

Timu Ya Raga Wachezaji 15 Kila Upande Ya Tamba Madagascar.

Timu ya Kenya ya raga wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 katika kitengo cha wachezaji 15 kila upande wameletea sifa taifa la Kenya baada ya kuwabamiza Madagascar 51-13  katika uga wa Hage Geingob Windhoek, nchini Namibia nakutinga fainali ya mashindano ya Barthes Cup.

Vijana hao walitawala mchezo huo kwani katika nusu ya kwanza ya mchezo waliongoza alama 27-13 na katika nusu ya pili walibamiza alama 14 na kuibuka na ushindi huo mnono.

Katika fainali itakayosakatwa jumamosi hii vijana hao wanaofunzwa na Paul Odera wanatarajiwa kukutana na aidha Namibia ama Zimbabwe

Atakaye shinda kipute hiki atapambana na mshindi wa eneo la kaskazini mwa afrika ili kupata nafasi ya kuwakilisha Afrika katika mashindano ya dunia ya vijana.

Show More

Related Articles