HabariPilipili FmPilipili FM News

Lori Za Kuvuna Mchanga Zanaswa Taita.

Lori 4 pamoja na trakta zinazuiliwa na polisi kaunti ya Taita-taveta  baada ya kubainika kuwa zilikuwa zinatumiwa kuvuna mchanga kimagendo katika mto Paranga.

Hii ni kufuatia oparesheni ya pamoja inayoendeshwa na maafisa wa polisi na wale wa kaunti, kwa ushirikiano na maafisa shirika la kutunza mazingira nchini NEMA.

Wakati wa oparesheni hiyo polisi pia wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu kadha, wanaoaminika kuendesha biashara ya mchanga kimagendo.

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta aliamuru kusitishwa kwa shughuli zote ikiwemo uvunaji wa mchanga hadi pale kaunti itakapotengeneza sheria za kudhibiti sekta hiyo.

Show More

Related Articles