HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Sokomoko yashuhudiwa katika ofisi inayohusiana na vyeti,Kericho

Sokomoko ilitanda katika ofisi ya serikali inayohusika na masuala ya vyeti vya kuzaliwa katika eneo la Kericho baada ya wazazi kulalamikia kuwepo kwa utepetevu na ufisadi katika kupokea stakabadhi hizo muhimu.
Wazazi hao walilalama kwamba hali hiyo itawapelekea wengi kutofikisha vyeti hivyo shuleni kwa wakati unaofaa, hivyo basi kuzuia wanao katika darasa la nane na kidato cha nne kutojisajili kwenye mfumo wa kuwatambua wanafunzi.
Katika kaunti ya Kakamega mamabo yalikuwa vivyo hivyo wazazi wakisalia kwenye foleni siku nzima na kulalamikia kulaghaiwa na watu katika ofisi hizo.

Show More

Related Articles