HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Viongozi magharibini mwa Kenya wapania kuunda chama kimoja kutetea maslahi ya jamii

Mgawanyiko sasa unanukia ndani ya muungano wa upinzani NASA, baada ya viongozi wa chama cha ANC na kile cha Ford Kenya kutoka magharibi mwa Kenya, kutishia kubuni chama kimoja watakachotumia kama umoja wa jamii za mulembe na wenzao wanaoishi maeneo hayo, kujipigia debe kisiasa na kimaendeleo.
Japo wajumbe hao wamesema kuwa chama hicho hakitakuwa cha kijamii bali chenye sura ya kitaifa, wao wamesisitiza kuwa wamechoshwa na wanasiasa ambao wamekuwa wakishirikiana nao kutoka maeneo mengine kisha wanawatema wana magharibi.

Show More

Related Articles