HabariPilipili FmPilipili FM News

Ajali Ya Ndege Yajeruhi Wawili Voi.

Watu wawili wanauguza majeraha  katika  hospitali ya Wesu eneo  bunge la Wundanyi   baada ya  ndege waliyokuwa wameabiri kuanguka  katika  eneo la  Kamang’ombe Kungu eneo  bunge la Mwatate.

Haya yamethibitshwa na OCPD wa Mwatate Francis  Mwangi na kuongeza  ndege hiyo ndogo ilikuwa  na watu  2 pekee kabla ya tukio hilo.

Majeruhi  wamekimbizwa na wasamaria  wema  katika hospitali ya Wesu wanakoendelea kupata matibabu huku kiini kilichopelekea ajali kikiwa bado kubainika.

 

Show More

Related Articles