HabariMilele FmSwahili

Kaunti ya Nyeri yapokea dawa zenye thamani ya milioni 64 kutoka shirika la KEMSA

Kaunti ya Nyeri imepokea dawa za thamani ya shilingi milioni 65 kutoka kwa shirika la kusambaza dawa KEMSA. Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga anasema hatua hiyo itasaidia kupunguza uhaba wa dawa katika hospitali za umma kaunti hiyo. Anasema dawa hizo zitasambazwa katika hospitali zote za umma.

Naye naibu mkurugenzi wa KEMSA Waiganjo Karanja anasema hospitali za umma kwenye kaunti zinadawa takriban shilingi bilioni 2.

Show More

Related Articles