HabariPilipili FmPilipili FM News

Paul Kihara Aidhinishwa Na Bunge.

Wabunge wameidhinisha uteuzi wa jaji Paul Kihara Kariuki kuchukua wadhfa wa mwanasheria mkuu nchini.

Akiongea wakati wa kikao cha kudhinisha uteuzi huo kiongozi wa wengi Aden Duale amesema Jaji Kihara amekuwa kielelezo katika masuala ya Sheria na idara ya mahakama, wakati akihudumu kama rais wa mahakama ya rufaa nchini.

Mbunge wa Suba John Mbadi ameunga mkono uteuzi huo na kumuomba jaji Kihara aishauri vyema serikali.

Akitolea mfano kuzuiliwa kwa wakili Miguna Miguna katika uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Mbadi anasema hatua hiyo imechangiwa na serikali kukosa washauri.

Bunge pia limejadili ripoti kuhusu uteuzi wa Noordin Mohamed anayetarajiwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma, iliyoachwa wazi na Keriko Tobiko ambaye sasa ni waziri wa mazingira.

 

Show More

Related Articles