HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazazi Wahimizwa Kutowaficha Watoto Walemavu Taita.

Wito umetolewa kwa familia  zinazoishi watu wenye ulemavu kutowafungia nyumbani na badala yake kuwatoa ili wafaidike na huduma mbali mbali  kutoka kwa serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Haya ni kulingana na mkewe gavana wa kaunti ya Taita Taveta Stella Samboja,ambaye amelaani dhana  ya baadhi ya watu katika jamii kwamba mtoto mlemavu hana haki ya kupata huduma za afya  na masomo, akisema mazingira yao yanafaa kuboreshwa.

Katibu wa afya katika kaunti hiyo Frank Mwangemi ameiomba serikali ya kaunti   kutenga fedha za kutosha, ili kusaidia idara za kushughulikia changamoto zinazowakumba walemavu kwa sasa.

Show More

Related Articles