MichezoPilipili FmPilipili FM News

Felmas Ndiye Mwanamichezo Bora Wa Mwezi Februari.

Felmas Adhiambo ndiye mwanamichezo bora wa mwezi Februari.

Felmas ambaye ni mchezaji wa kilabu ya bandari ya mchezo wa vikapu wa upande wa kinadada.Mchezaji huyo ambaye alitamba kwenye ligi ya mpira wa vikapu msimu uliopita amewapiku wenzake saba ambao walikua wakishindana kwenye tuzo hio.

Mchezaji huyo amewashukuru wakufunzi na wachezaji wenzake kwa kufanikisha mafanikio yake huku akiongeza hakuwa na ufahamu wakutuza tuzo kubwa kama hio kwani yeye anaupenda mchezo huo kwa moyo na hakuna siku aliwazia kuja kuchaguliwa mchezaji bora.

Wakati huo huo amedokeza ndoto yake yakuchezea moja wapo ya vilabu vya Afrika Magharibi hususani nchini Angola akisema yeye huvutiwa na ushindani wa mataifa ya ukanda huo.

Ameweza kutunukiwa hundi ya shilingi laki moja,kikombe na runinga ya upana wa nchi 42 na kampuni ya Startimes

Tuzo hio imetolewa kwa hisani ya muungano wa waandishi wa michezo nchini SJAK pamoja na kampuni ya Startimes.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kupeana tuzo hio mkurugenzi wa uhusiano mwema wa kampuni ya Startimes Alex Mwaura amesema nia yao kubwa nikuhakikisha wanamichezo wanapewa motisha yakujizatiti michezoni na kuona matunda ya ufanisi wao wa kimichezo.

Show More

Related Articles