People Daily

Maafisa Elfu Tisa Wa G.S.U Wafuzu

Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza hafla ya kufuzu kwa takriban maafisa elfu 9 wa GSU katika chuo cha mafunzo ya maafisa hao Embakasi jijini Nairobi.

Akiongea wakati wa hafla hiyo rais Kenyatta amedokeza kuwa maafisa wanaofuzu leo wamepewa mafunzo maalum kulingana na mtaala mpya wa mafunzo ya maafisa wa usalama, ambayo yatawasaidia kukabiliana na hali zote zinazoweza kuhatarisha maisha ya wakenya na mali zao kwa ujumla.

Rais amepongeza utendakazi wa maafisa wa usalama katika mchango wao kwa taifa, akisema serikali itaendelea kuboresha mazingira yao ya kazi, ikiwemo kuwapa vifaa hitajika, bima za afya na maakazi bora, ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo

Show More

Related Articles