MichezoPilipili FmPilipili FM News

Rais Ayaonya Mashirikisho Ya Michezo Nchini.

Rais Uhuru Kenyatta ameyataka mashirikisho yote ya michezo humu nchini kuhakikisha kuwa yanawashughulikia wanamichezo vizuri.

Rais amedokeza kuwa mashirikisho yanajukumu lakuhakikisha timu za michezo zinapata malipo bora,maandalizi mema,na vifaa bora vya michezo wakiwa humu nchini ama katika mataifa ya nje.

Kila kitu tunachokubaliana lazima kitimizwe nimeshangazwa kuona kuwa kuna vitu ambavyo havijatimizwa. Amesema rais Kenyatta.

Aliyasema hayo wakati akiikabidhi bendera timu itakayoiwakilisha Kenya katika mashindano ya jumuia ya madola jijini Gold Coast nchini Australia.

Bendera hio ilikabidhiwa nahodha wa kikosi hicho Elijah Manangoi.

Amesema mashirikisho ya riadha ,golf,soka,raga,kriketi na hockey yanafaa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kutimiza majukumu yao kikamilifu.

Huku akionya hatokubali wanamichezo wakiteseka akiangalia.

Rais amemtaka waziri wa michezo Rashid Echesa kuhakikisha timu hiyo inaoata maangalizi bora na inalipwa marupurupu yao.

Kenya itawakilishwa na wanamichezo 300 katika mashindano hayo yatakayoanza Aprili 4 hadi 15 mwaka huu.

 

Show More

Related Articles