HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Machifu Wajir wameanza kujitwika majukumu ya kufunza shuleni

Kaunti ya Wajir imelazimika kujihami kwa mbinu mbadala kukabiliana na uhaba wa walimu.
Sasa chifu wa eneo la Argani Noor Abdi, amevua gwanda la chifu,na kuwa mwalimu, kujaribu kutatua uhaba ulioshuhudiwa zaidi ya mwezi mmoja tangu tume ya kuwaajiri walimu nchini, tsc kuamua kuwahamisha walimu 900 wasiowenyeji.
Pia kuna waalimu ambao wamepiga moyo konde na kuzidi kutekeleza wajibu wao wa kuwapa wanafunzi wa eneo hilo la kaskazini mwa nchi elimu licha ya taharuki ya kiusalama inayowakodolea macho kila uchao hasa baada ya walimu watatu kuuawa kufuatia mashambulizi ya kigaidi Wajir.

Show More

Related Articles