HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wazazi wazidi kuhangaika kupata vyeti vya wanao kuzaliwa

Maelfu ya wazazi wanazidi kuhangaika kwenye afisi za serikali zinazoshughulikia masuala ya vyeti vya kuzaliwa, huku makataa ya siku thelathini zilizoongezwa na serikali ili wazazi wawasilishe stakabadhi hizo shuleni yakikamilika mwishoni mwa juma.
Zaidi ya wanafunzi 18,000 bado hawajapata stakabadhi hizo katika kaunti ya Bungoma pekee, huku walimu katika kaunti za Kiambu na Nairobi wakilalama kuwa matapeli wanawalaghai wazazi na kuwauzia stakabadhi ghushi.
Frankline Macharia anasimulia kuhusu taabu na matatizo wanayopitia wazazi.

Show More

Related Articles