HabariMilele FmSwahili

IPSOS : Kinyanganyiro cha urais mwaka wa 2022 kitakuwa kati ya William Ruto na Seneta Gedion Moi

Kinyanganyiro cha uchaguzi wa urais mwaka wa 2022 kitakuwa kati ya naibu wa rais William Ruto na seneta wa Baringo Gedion Moi. Hii ni kulingana na utafiti wa shirika la IPSOS Synovate unaoonyesha kinara wa NASA Raila Odinga huenda akawa wa nne kwenye kinyanganyiro hicho. Utafiti huo unaonyesha kuwa Ruto huenda akachukua uongozi wa nchi baada ya kuondoka kwa rais Uhuru Kenyatta akiongoza kwa aslimia 30. Tom Wolf mtafiti mkuu kwenye shirika hilo anasema gavana wa Mombasa Hassan Joho ni wa tatu . Gavana wa Machakos Alfred Mutua anachukua nafasi ya mwisho kwenye orodha ya wanaomezea mate kiti hicho. Kwenye utafiti huo wakenya pia wameelezea hisia zao kuhusu jinsi hali ilivyo nchini.

Show More

Related Articles