HabariPilipili FmPilipili FM News

EACC Yakiri Kupiga Hatua Kukabiliana Na Ufisadi Nchini.

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imeeleza kupata mafaniko makubwa katika juhudi zake za kukabili ufisadi nchini.

Eliud Wabukala ambaye ni mwenyekiti wa tume hiyo, anasema mwaka jana wa 2017 pekee walifanikiwa kushughulikia zaidi ya kesi 25 mahakamani, tofauti na miaka michache iliyopita ambapo ni kesi moja tu iliyoshughulikiwa mwaka wa 2013.

Anasema pia wamefanikiwa kutwaa mali yenye thamani ya shilingi bilioni 6.7, iliyokuwa ikishikiliwa na wafisadi katika maeneo kadha ya nchi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Halaqe Wako amewataka wakenya wote kuchukua jukumu la kupambana na ufisadi, akisema ni vigumu kukabili ufisadi bila kuwepo ushirikiano mzuri.

Wawili hao wameongea haya wakati wa kutoa ripoti ya tume hiyo kuhusu hatua zinazofanywa kukabili ufisadi.

 

 

Show More

Related Articles