HabariPilipili FmPilipili FM News

Ombeta Asistiza Miguna Ni Mkenya Halali.

Wakili Miguna Miguna amekataa kutotia saini stakabadhi za idara ya uhamiaji , kabla ya yeye kuruhusiwa kukaa nchini.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Nairobi wakili wake Cliff Ombeta amesema mteja wake hatosaini stakabadhi hizo, akisema zinakiuka haki zake na kusistiza kuwa Miguna ni raia halali wa Kenya hivyo hapaswi kujisajili upya kama mkenya.

Wakati huohuo wakili Ombeta amedai hawajaruhusiwa kumuona Miguna baada ya kuachana jana usiku pale alipokatalia kusafirishwa hadi nchini Dubai.

Ikumbukwe kuwa Miguna alirudishwa nchini kutoka Canada jana adhuhuri baada ya kufurushwa na serikali mwezi mmoja uliopita.

 

 

 

 

Show More

Related Articles