HabariMilele FmSwahili

EACC: Kaunti ya Muranga inaongoza kwa visa vya ufisadi nchini

Kaunti ya Muranga inaongoza kwa visa vya ufisadi nchini ikifuatiwa na Transnzoia. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na tume ya kukabiliana na ufisadi mwaka wa 2016, Mandera Kirinyaga na Lamu ni miongoni mwa kaunti zenye viwango vya chini vya ufisadi. Utafiti huo pia umebaini kuwa utoaji hongo umekithiri katika kaunti asilimia 46 ya wakenya wakikiri kutoa rushwa. Aidha matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa na afisa mkuu Halakhe Waqo yanaashiria kuwa wizara ya usalama wa ndani pamoja na ile ya afya zina visa vya juu vya ufisadi. Idara ya polisi imetajwa kuwa fisadi mno asilimia 10 ya wakenya wakihisi kuwa serikali haijaweka mikakati mwafaka kukabili jinamixzi hilo. Naye mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukhala amewahimiza wakenya kutilia maanani mchango wao katika kukabili ufisadi.

Show More

Related Articles