HabariMilele FmSwahili

Kiwango cha mvua inayonyesha nchini kupungua siku saba zijazo

Mvua inayonyesha nchini inatarajiwa kupungua katika kipindi cha siku saba zijazo. Katika taarifa shirika la utabiri wa hali ya hewa imedokeza mvua chache itashuhudiwa katika maeneo mengi isipokuwa mashariki kati ya leo na tarehe 2 Aprili. Shirika hilo limesema kuwa kaunti za Siaya, Kisumu, Homabay, Migori, Kisii, Nyamira, Transnzoia, Baringo, na Uasingishu pamoja na Bungoma zitashuhudia mvua chache. Maeneo mengine ambako mvua itapungua ni katika kaunti za Nairobi, eneo la mlima Kenya kaskazini mashariki na Pwani

Show More

Related Articles